Barcelona yamuwinda nyota huyu wa Man City, nyota wengine wanaotikisa usajili hawa hapa

 


Barcelona wamefanya mazungumzo na wakala wa mchezaji wa Manchester City, Eric Garcia siku ya Jumatano kwaajili ya kuona uwezekano wa kumsajili nyota huyo raia wa Hispania.

Beki huyo wa kati wa City, Eric Garcia huwenda akarejea Camp Nou mahala ambapo aliondoka mwaka 2017 lakini kwa mujibu wa ripoti ya El Mundo Deportivo inadai kuwa mshahara aliyoandaliwa huwenda ukawa ndiyo kikwazo cha usajili huo.

Juventus inataka kusaini upya mkataba na mshambuliaji wa Everton na Italia Moise Kean, ambaye yuko katika mkataba na Paris St-Germain. The Toffees wanataka euro milioni 50 (£43.5m) kwa ajili ya Kean, 21, au mkataba wa kubadilishana wachezaji unaomuhusisha kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 26, au kiungo wa kati-nyuma wa Uturiki Merih Demiral, 23. (Gazzetta – in Italian)



Kiungo wa safu ya kushoto-nyuma wa Juventus Brazil Alex Sandro

Chelsea wanaangalia uwezekano kubadilishana wachezaji kati ya kiungo wa safu ya kushoto-nyuma wa Juventus Brazil Alex Sandro, 30, na Muitalia Emerson Palmieri anayecheza katika safu ya nyuma-kushoto, 26. (Calciomercato – in Italian)



Post a Comment

Previous Post Next Post